Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh. William Lukuvi
amepiga marufuku wananchi kuuza ardhi kwa wawekezaji wa kigeni.
Ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilaya Magu
mkoani Mwanza kwaajili ya kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka
30.
“Iko tabia na mazoea ya nchi hii,nyinyi wananchi wengi wa vijijini
mmekuwa mnawaruhusu sana hawa wananchi wanaojiita wawekezaji, na wengi
wao wanaokuja kununua ardhi kwa mtindo huu ni aina ya watu waliokuja
kununua mwaka 84, hawa hawa watanzania wenye asili ya Asia mliowapa
nyinyi, wananunua ardhi kwenu hawaendelezi, ardhi ile wanachukulia
mapesa benki wanafika mahali halafu baadaye wanakuja kuuza,” alisema
Lukuvi.
“Mtu yeyote leo ni marufuku kwa serikali ya wilaya kumkubalia au watu
wangu wa wizara ya ardhi mtu yeyote hajaendeleza shamba ambaye
hajaendeleza shamba amekaa nalo kwa miaka kumi hajaendeleza, halafu kwa
ujanja ujanja anataka kuliuza kwa mtu mwingine au kulitumia kwa njia
nyingine kutengeneza sijui viwanja na nini ni marufuku,” alionya.
No comments:
Post a Comment