Latest News

Monday, March 6, 2017

Yanga wapigwa faini ya laki tano



Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Tanzania (Kamati ya Saa 72), katika kikao chake cha Machi 4, 2017 iliptia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 inayoendelea hivi sasa.

Katika mechi namba 169 kati ya Simba na Young Africans iliyochezwa Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Young Africans iliingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.

Kitendo hicho ni kwenda kinyume cha kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu inayoelekeza kuwa timu zitaingia uwanjani kwa kutumia milango rasmi.

Hivyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14 (48) ya Ligi Kuu, Kamati imeipiga Young Africans fainali ya Sh 500,000 (lakini tano).

Katika kikao hicho kilifuta kadi ya kwanza ya njano aliyoadhibiwa mchezaji Obrey Chirwa wa Young Africans wakati timu hiyo ilipocheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Machi mosi, mwaka huu.

Kadi hiyo imefutwa kwa mujibu wa kanuni ya 9 (8) baada ya Kamati ya Saa 72 haikupaswa kutolewa kwa Chirwa kwa sababu hakukuwa na kosa wala mazingira ya kuonywa.

No comments:

Post a Comment