Watu 20 wamefariki dunia papo hapo baada ya basi moja la watalii
kuanguka kutoka juu ya mwamba karibu na eneo la kujivinjari lililopo
Kusini mwa Uturuki.
Watu wengine 11 walijeruhiwa wakati dereva alivyopoteza mwelekeo wa basi hilo dogo na kugonga kizuizi.
Vyombo vya habari nchini Uturuki vimesema kuwa hakuna watalii wa kigeni waliokuwemo katika basi hilo.
Takriban
watu 400 walikuwa wameabiri basi hilo kulingana na gavana wa mkoa wa
Mugla, Amric Cicek ambaye anasema huenda breki zilifeli.
Lakini
Meya wa eneo la Marmaris, Ali Acar aliambia gazeti la Uturuki la
Hurriyet akisema ajali hiyo ilisababishwa na makosa ya dereva.
Vyombo vingine vya habari vinasema kuwa waathiriwa wengi walikuwa wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment