Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema amesikitishwa na
hatua ya Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam ya kuzuia kongamano la
demokrasia lililopangwa kufanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa
Anatouglou.
Lowassa ambaye ni
mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alitoa kauli hiyo leo (Jumamosi) wakati
akizungumza na wanahabari ofisi kwake Mikocheni.
Amesema
amelaani kitendo hicho na kusema kongamano hilo halikuwa na nia mbaya
bali lilikuwa limelenga kujadilia mambo mbalimbali kwa mustakabali wa
Taifa.
"Nimesikitishwa na kitendo hiki na nimeshangaa kwa jambo hili halikemewi.Nchi hii ni moja na kila mtu ana haki.
"Walituzuia
mikutano ya hadhara tumetii, tumeamua kufanya mikutano ya ndani
wanatufuata fuata,"amesema Lowassa ambaye aliwahi Mbunge wa Monduli kwa
nyakati tofauti.
Katika mkutano huo
Lowassa aliambatana na mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya kongamano
hilo Dk Makongoro Mahanga ambaye alishangazwa na hatua hiyo ya Serikali
ya mkoa wa Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment