Aliyekuwa Mwandishi wa habari wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere, Paul Sozigwa anatarajiwa kuzikwa Jumanne ya wiki ijayo
Kisarawe mkoani Pwani.
Sozigwa alifariki jana katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,(JKCI) alikokuwa akitibiwa.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa familia ya marehemu
Sozigwa, Mokile Ismail alisema kuwa misa pamoja na kuuaga mwili
vitaanza Jumatatu saa sita mchana nyumbani kwa mwanae Mtoni Mtongani.
Amesema misa nyingine itafanyika Kisarawe siku ya Jumanne ambayo pia ndiyo siku atakayopumzishwa kwenye nyumba ya milele.
“Tutauaga
mwili hapa siku nzima ya Jumatatu na mwili utalala hapa nyumbani
kwangu, kabla ya kusafirisha kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika
Kisarawe ambako pia kutakuwa na misa, ”amesema Mchungaji Moses Sozigwa
ambaye ni mtoto wa marehemu Sozigwa
No comments:
Post a Comment