Msanii Ben Pol amezungumza kuhusu picha yake ya utupu iliyozua maswali mengi na kusababisha kuleta picha mbaya kwenye jamii.
Kupitia AyoTv Ben Pol amesema kuwa yeye kama msanii anapaswa kuelezea kitu kwenye ukweli ili kuonyesha uhalisia kupitia sanaa yake. Ben Pol amesema kuwa Msanii anatakiwa kuzingatia vitu kadhaa katika kuonyesha uhalisia ikiwemo haki, uwazi na mazingira halisi hususan kwa picha aliyoiwekwa.
Ben Pol alisema kuwa Wazazi walimpigia simu na kuuliza kuhusu usalama wake hususan mama yake ambaye hakupata usingizi.
"Baba yangu alinipigia simu akaniambia vipi mwanangu uko wapi, uko salama kweli?". Alisema Ben Pol.
Aidha Ben Pol amesisitiza kuwa hiyo ni Project yake mpya inayokuja ambayo kabla hajafanya hivyo amesema kuwa project hiyo imeshapitiwa na watu si chini ya watano ili waweze kuiruhusu kuweza kuweka kwenye mtandao wa Instagram na sehemu nyingine.

No comments:
Post a Comment