Latest News

Tuesday, June 6, 2017

Bi Anna Mghwira Amshukuru Rais Magufuli Kwa Kuteuliwa Kuwa Mkuu Wa Mkoa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Juni, 2017 amemuapisha Bibi Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Bibi Anna Elisha Mghwira amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo.

Kwa upande wake Rais John Magufuli ameeleza sababu ya kumteua Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro huku akimhimiza akachape kazi.

Rais Magufuli ametaja sababu hiyo wakati wa hafla ya kumwapisha Mghwira iliyofanyika leo, Jumanne jijini hapa na kuhudhuriwa na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
“Mimi huwa siteui watu hivi hivi, huwa naangalia uwezo wa mtu na wewe nimekuchunguza na nimejiridhisha kuwa una uwezo wa kuwatumikia wananchi, nenda kachape kazi, kawaondolee kero wananchi wa Kilimanjaro,”amesema Rais Magufuli na kuongeza;
“Wapo watu watakaokusema na wengine watakuonea wivu, wewe kachape kazi.”
Rais Magufuli amemhakikishia kuwa atapata ushirikiano wa kutosha wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake na asikubali kuyumbishwa na mtu yeyote katika majukumu yake.

No comments:

Post a Comment