Mfanyabiashara na kada maarufu wa CHADEMA Yericko
Nyerere amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akikabiliwa na mashtaka matano ya kutoa taarifa za upotoshaji kupitia mtandao
wa Facebook.
Kwa mujibu wa kesi hiyo namba 184, 2017, Wakili
wa Serikali, Elia Athanas alidai kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri kuwa
mshtakiwa huyo alifanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya
Mtandao Namba 14 ya 2015
Ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha
masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye amesaini bondi ya Sh 10milioni.
Kesi imeahirishwa Juni 5, 2017 kusomewa maelezo
ya awali (PH).

No comments:
Post a Comment