Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini
kutumia weledi wake kwa kiwango cha juu katika kutekeleza jukumu lake lakulinda
raia na mali zao, hasa kukomesha vitendo vya uhalifu.
Mhe.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 02 Juni, 2017wakati akizungumza na
Makamanda Wakuu kutoka makao makuu ya polisi, Makamanda wa Mikoa na Vikosi vya
Tanzania Bara na Zanzibar na viongozi wote wakuu wa polisi wa Mkoa wa Dar es
Salaam waliokutanakatika Bwalo la Maofisa Wakuu wa polisi lililopo Oysterbay
Jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Dkt. Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa juhudi zake za kukabiliana na
uhalifu lakini ametaka juhudi hizo ziongezwe hususanikukabiliana na matukio ya
ujambazi na mauaji ya raia, dawa za kulevya na kuendesha operesheni zenye tija
katika mikoa yote.
Amemuagiza
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kujipanga vizuri yeye na safu
yake ya Makamanda, Viongozi Wakuu wa Vikosi na Maofisa mbalimbali ili kuondoa
dosari zote za utendaji kazi zinazoshusha ufanisi na heshima ya Jeshi la
Polisi.
“Ni
lazima ufanye mabadiliko makubwa, nataka kuona Jeshi la Polisi linakuwa Jeshi
la Polisi, Wewe IGP Sirro na Makamnda wenzako hakikisheni mnakomesha uhalifu,
komesheni mauaji dhidi ya raia, ujambazi na dawa za kulevya” amesema Mhe. Rais
Magufuli.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amewataka Makamanda, Maofisana Askari wa jeshi hilo
kujiepusha na rushwa, dawa za kulevya, kutumiwa na watu kwa maslai binafsi,
kuingia mikataba isiyo na maslai kwa Jeshi na Taifa, ubadhirifu na kuacha
upendeleo katika utoaji wa ajira na vyeo.
Mhe.
Rais Magufuli pia ametaka Makamanda, Maofisa na Askari wote wa Jeshi la Polisi
wampe ushirikiano wa kutosha IGP Simon Sirro ambaye hivi karibuni amemteua kuwa
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Kikao
hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck
Nchemba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali
Mstaafu Projest Rwegasira.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
02
Juni, 2017

No comments:
Post a Comment