Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesema Serikali imebaini kiini cha mauaji, yanayotokea mkoani Pwani na imeanza kuchukua hatua za kudhibiti watu wanaohusika na mauaji hayo.
Waziri Mwigulu ametoa hauli hiyo kwenye mikutano aliyoifanya maeneo mbalimbali, wilaya ya Iramba mkoani Singida, ambapo amehusisha mauaji hayo, na chuki za kisiasa zinazofanywa na baadhi ya vyama vya siasa, kwa lengo la kuwatisha wananchi ambao si wafuasi wa vyama hivyo hususani wanachama wa Ccm.
Mauaji haya yanasadikiwa kufanywa na kikundi kimoja cha watu, ambapo maeneo ambayo yamekuwa yakishambuliwa zaidi katika mkoa huo ni wailaya za Kibiti naRufiji.
Aidha waziri Mwigulu amesema Serikali ya sasa haipo tayari kucheza mchezo wowote mchafu, na kudai kuwa kuanzia sasa watanzania hususan wakazi wa mkoa wa Pwani, wasubiri kuona kazi inayofanywa na Serikali.
No comments:
Post a Comment