Mkuu wa jeshi la Polisi nchini IGP Sirro amewataka waandishi wa habari kuzingatia uzalendo wanaptekeleza majukumu yao, hususan katika kuripoti matukio ya mauaji, ili kuondoa hofu miongoni mwa jamii.
Sirro ameyasema hayo mjini Morogoro, wakati akizungumza na maafisa wa jeshi hilo, na baadaye kuzungumza na waandishi wa habari, huku akiwapongeza kwa ushirikiano wao, kwa jeshi la polisi.
IGP Sirro amezungumzia pia suala la mauaji yanayoendelea Kibiti na Ikwiriri mkoani Pwani, ambapo amewataka wananchi kuwa watulivu wakati jeshi la polisi likiendelea na kazi yake hususan uchunguzi juu ya matukio yanayoendelea kutokea katika maeneo hayo.
Hii hapa chini ni taarifa kamili:-
No comments:
Post a Comment