Latest News

Friday, June 2, 2017

Imebainika: Grezieman Akandamiza Kibabe Kwenye Maumivu Ya Manchester United


Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu mchezaji Antoine Griezman kuhusiana na uhamisho wake wa kwenda Manchester United.
Griezman mwenyewe alisema wazi kwamba kuna alama 6 kati ya 10 kwamba yeye anakwenda United na kuifanya dunia iamini kwamba kweli Griezman anatua Old Trafford.
Lakini tweet ya mchezaji huyo imebadilisha kabisa upepo wa habari yake na kuanza kuipeleka katika upande mpya kwani Griezman anaonekana kubaki Atletico Madrid.
Griezman aliandika “now more then ever” na kuweka hashtags ambazo zilionesha umoja alionao yeye na klabu yake ya sasa ya Atletico Madrid.
Taarifa toka ndani ya klabu ya Manchester United zinasema United tayari wameona dili hilo ni gumu kwa sasa na wameanza kuangalia uwezekano wa nyota mwingine mkubwa.

No comments:

Post a Comment