Latest News

Tuesday, June 6, 2017

Jokate Alitoa Machozi Kwa Uchungu!


Mjasiriamali na mwanamitindo maarufu nchini Tanzania, Jokate Mwegelo amedai kitu ambacho kimemtoa machozi hivi karibuni ni jinsi mama yake anavyotumia nguvu kubwa kumuuguza baba yake ambaye anaumwa kwa muda mrefu.
Mrembo huyo ambaye ametajwa katika orodha la jarida la Forbes Africa la kuwa miongoni mwa vijana walio na umri chini ya miaka 30 wenye mafanikio mbalimbali kwa mwaka 2017, alisema hayo baada ya kuulizwa ni kitu gani hivi karibuni kimemtoa machozi.
“Kusema kweli hivi karibuni nimelia sana, baba yangu anaumwa sasa mama yangu anatumia nguvu kubwa kumuudumia kwa sababu baba anahitaji uangalizi wa karibu sana,” Jokate aliimbia MCL.
Pia mwanamitindo huyo amedai kwa sasa anatamani kuwa na familia lakini bado hajajua ni lini.

No comments:

Post a Comment