Mjadala wa mchanga wa dhahabu (makinikia) umeibuka tena bungeni mbunge akiwatuhumu wenzake, huku akimtetea Profesa Sospeter Muhongo kuwa ametolewa madarakani kama vile mbuzi wa kafara.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea amesema Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa wawajibike kwa kuwa ni wahusika wa mikataba mibovu ya madini.
Amesema makinikia yana dhahabu lakini yanayofanyika yanaweza kuliingiza Taifa kwenye mgogoro wa kidiplomasia, kisheria na wa kimahakama.
Kubenea ametoa shutuma hizo leo (Ijumaa) akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/18.

No comments:
Post a Comment