Latest News

Wednesday, May 31, 2017

IGP Sirro, Aweka Wazi Vipaumbele Vyake Vitano!!!


Baada ya Kuapishwa IGP Simon Sirro ameamua kuzungumza na waandishi wa habari mikakati amabayo ataanza nayo katika kufanyia kazi ambapo akazungumzia suala la mauaji ambayo yamekua yakiendelea mkoani Pwani ikiwemo maeneo ya Ikwiriri, Kibiti na Rufiji.

IGP Sirro amesema kuwa ni lazima majibu yapatikane ndani ya muda mfupi kwani anaamini ushirikiano katika kuweza kuibua ubaya huu upo wa kutosha na kwamba suluhisho lazima lipatikane.

Aidha IGP Sirro amewazungumzia madereva bodaboda katika upande wa mkoa wa Dar Es Salaam ambao wamekuwa hafuati alama za barabarani pamoja na upakiaji wa mshikaki ambapo amesema suala hilo lazima lifanyiwe kazi.

IGP Sirro amegusia suala la madawa ya kulevya, kwa kusema oparesheni bado inaendelea huku katika suala la wananchi kujichukulia sheria mkononi katika masuala mbalimbali IGP Sirro amesisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kuacha vitendo hivyo mara moja kwani vinaweza kuwagharimu kuanzia sasa.

Sirro amesema katika mapitio aliyoyafanya amegundua takribani matukio 40 ya mauaji ya hasira kali yametokea kuanzia mwaka jana mpaka mwaka huu kwa kipindi kama hiki, na kwamba waliokufa mwaka jana na  mwaka huu ni zaidi ya mia mbili.

IGP amesema kuwa Rushwa ni adui wa haki hivyo kwa kutambua hilo atasimamia kwa weledi suala hilo lisiwepo hususan askari ambao wamekuwa wakipokea rushwa kwamba waache mara moja huku akiwasisitiza wananchi pia waweze kuacha kuwashawishi akari hawa kupokea Rushwa kwani ni vitendo visivyokuwa na maadili katika nchi ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment