Latest News

Wednesday, May 31, 2017

Imebainika, Ndesamburo Alifariki Alipofika Kazini Tu, R.I.P


Mbunge wa zamani wa jimbo la Moshi mjini, na mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo, Chadema mkoani Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo, amefariki dunia muda mfupi baada ya kufika ofisini kwake, jana asubuhi, ambapo alikuwa akijiandaa na majukumu yake ya kila siku.

Taarifa za mapema zinaeleza kuwa mzee Ndesamburo amefariki jana jumatano majira ya saa nne asubuhi akiwa katika kitengo cha wagonjwa wa dharula katika Hospitali ya KCMC Moshi, ambapo alipelekwa kwaajili ya matibabu, baada ya hali yake kubadilika ghafla mara baada tu ya kufika ofisini.
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Bazil Lema amesema mwili wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Moshi mjini Phillemon Ndesamburo unafanyiwa uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo chake cha ghafla na kuongeza kuwa Ndesamburo alifika ofisini kwake asubuhi  kama ilivyo kawaida yake  lakini aliugua ghafla mnamo saa nne asubuhi.

Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi, Raymond Mboya, ameeleza kuwa moja ya majukumu aliyokuwa nayo Marehemu siku ya jana ni pamoja na kukabidhi hundi ya rammbirambi, kwa wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Luck Vicent, ya jijini Arusha.

Mtaalamu wa magonjwa ya binadamu na ngozi wa hospitali ya KCMC Profesa Elisante Masenga, ameelezea sababu za kifo cha mzee Ndesamburo 
 , huku Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, ametuma salamu za rambi rambi kwa familia ya marehemu Philemon Ndesamburo, viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na kifo hicho.



No comments:

Post a Comment