Ofisa wa juu wa Ubalozi wa Marekani ana wasiwasi kutokana na
jinsi viashiria vinavyokatisha tamaa, kuonyesha kwamba Tanzania inarudi
nyuma katika masuala ya uwazi, haki za binadamu na utawala wa sheria na
kusema visiposhughulikiwa, vitaathiri biashara na nafasi ya nchi kama
kinara wa usalama.
Ofisa huyo, Virginia Blaser, Balozi
Mdogo wa Marekani Afrika Mashariki, alisema hayo katika mahojiano
maalumu na gazeti la The Citizen Alhamisi iliyopita, siku chache kabla
ya kumaliza kipindi chake cha miaka minne.
Alisema
wakati Serikali ikistahili pongezi kwa jitihada ilizoonyesha za
kupambana na rushwa, pia inatakiwa ichukue hatua kuendeleza uwazi na
utawala wa sheria na kuangalia ishara zinazotia shaka ya kurudisha nyuma
mambo, hasa sekta binafsi.
“Mustakabali wa Watanzania
hauwezi kutegemea wadau wa maendeleo; hautatokana na ajira za
serikalini; unatakiwa utoke katika sekta binafsi ambayo ni pana, imara,
yenye hali nzuri na inayoaminika,” alisema.
“Na badala yake, naona ishara zinazokatisha tamaa katika sekta binafsi; na nina wasiwasi Tanzania itachukua njia gani.”
Aliongeza
kuwa angependa kuona kampuni nyingi zaidi kutoka Marekani zikiingia
nchini, lakini hilo litategemea zaidi “mazingira ya uwazi na
yanayosaidia sekta binafsi”.

No comments:
Post a Comment