Latest News

Thursday, June 1, 2017

Hii Hapa Ratiba Ya Mazishi Ya Marehemu Ndesamburo


Wiki hii Taifa limekumbwa na msiba wa mwanasiasa mkongwe ambaye ni Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo aliyefariki dunia jana, taarifa iliyopo ni kwamba Ndesamburo atazikwa Jumanne ijayo.
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa ameliambia gazeti hili kuwa Ndesamburo atazikwa katika makaburi ya familia nyumbani kwake eneo la Mbokomu.
Golugwa amesema Jumatatu, Juni 5 kwenye viwanja vya mashujaa mjini Moshi wananchi watapata fursa ya kuaga mwili wa Ndesamburo.
Katibu huyo amesema wakati wa kuaga mwili wake kutakuwa na salamu kutoka kwa viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini na wawakilishi wa makundi mbalimbali.
Golugwa amesema msiba wa Ndesamburo umewagusa wengi nchini kutokana na mchango wake katika kukuza misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kuchangia ustawi wa sekta ya utalii.

No comments:

Post a Comment