Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewasimamisha kazi vigogo wawili hadi uchunguzi wa sakata la vitabu vya kufundishia utakapokamilika.
Waliosimamishwa
ni Kaimu Kamishna wa Elimu na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu
(TIA) ambayo ndiyo imepewa idhini ya kusimamia ubora wa vitabu.
Kauli
hiyo imetolewa bungeni leo (Jumatatu) kutokana na Mbunge wa Viti
Maalumu (CCM), Esther Mmasi kutoa hoja ya kushika shilingi katika
mshahara wa waziri akitaka uamuzi kuhusu suala hilo.
Hoja
hiyo iliungwa mkono na wabunge wa kambi zote bungeni wakiwamo, Philipo
Mulugo (Songwe -CCM), Peter Serukamba (Kigoma Kaskazini -CCM), Suzan
Lyimo (Viti Maalumu -Chadema) na Mwita Waitara (Ukonga -Chadema).
Profesa
Ndalichako akijibu hoja hizo, amesema ameunda tume kuchunguza suala
hilo na kuwahakikishia kuwa waliohusika hawako katika taasisi ya TIA.
“Nawahakikishia kuwa baada ya kukamilisha uchunguzi kila aliyehusika atabeba msalaba wake,” amesema.
No comments:
Post a Comment