Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa, Ritta Kabati amesimama jana Bungeni Dodoma na kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kuchangia kuhusu Benki ya wanawake kuweza kusaidiwa hususan ahadi ya serikali kusaidia Benki hii na kukidhi haja ya kila mwanamke kukidhi mahitaji kupitia Benki hiyo.
Aidha Kabati amesema Serikali ilitoa ahadi ya kutoa Ruzuku mwaka 2010, kila mwaka kutoa bilioni mbili kwa benki hii ya wanawake ila tangu ahadi ilipotolewa ni shilingi bilioni 5.75 ambayo imetolewa mpaka sasa hivi, hivyo akahoji kuwa pesa iliyobaki itatolewa lini.
Aidha Kabati akagusia benki ya TIB ( Tanzania Investment Bank ), akasema kuna umuhimu wa benki hii kuwezeshwa kwani ina msaada katika miundombinu ya viwanda, na imewezeshwa kwa kiasi kidogo tofauti na ilivyotakiwa hivyo akahoji serikali ina mpango gani wa kuiwezesha zaidi benki hii iendelee kufanya kazi.
Tizama video hapa chini.................................................

No comments:
Post a Comment